SALMA JABU NISHA
Huyu ni msanii wapekee mwenye mashabiki wengi hasa hasa watoto yeye ni msanii wa kuchekesha ila serious pia anaweza Game la comedy kwa upande wa wanawake yeye ndio amelikamatia kwa muda mrefu ameweza kuchukua tunzo za Action & Cut kwa mwaka 2013/14. Ni msanii mwenye maendeleo makubwa anamiliki kampuni yake mwenye ya filamu {NISHA'S FILMS PRODUCTION} ambayo imeshatoa filamu kama PUSI NA PAKU, TIKISA, GUMZO NA ZENA NA BETINA na hivi karibuni anatarajia kuachia movie yake mpya. Kama unampenda SALMA JABU NISHA nunua copy original ili kuendeleza sanaa ya Tanzania na kuongeza ajira kwa vijana
WASTARA JUMA
Huyu ni msanii ambaye naweza kusema ni shujaa kwani ameshakumbana na vikwazo vingi lakini ameweza kusimama na mpaka kupata tunzo ya msanii bora wakike ameshafanya kazi nyingi nzuri Team yake wanapenda kumuita SUPER WOMAN
SHAMSA FORD
Mwanadada huyu yeye analiteka jiji kwa staily yake yakubadilikabadilika kila kukicha ameweza kuwateka watu zaidi katika movie yake ya CHAUSIKU
No comments:
Post a Comment