Sunday, 21 June 2015

KIOO CHA JMII-NISHA BEBEE

Hii Ndioo Maana Ya Msemo Wa
Msanii Ni Kioo Cha Jamii
Namshukuru M/MUNGU kwa kuweza kutusaidia
kufanikisha jambo nililolipanga kuwa iwe
kawaida yangu kuwasaidia wale wenye matatizo
na waishio katika mazingira magumu napenda
kuwashukuru watoto wangu TEAM NISHA kwa
kujumuika nami jana bila kujali umbali
tuliokwenda pia natoa shukrani zangu za dhati
kwa vyombo vya habari.
Napenda kuongea jambo moja kuna watu
wanasema nikitoa mkono wa kushoto wakulia
usijue wakiwa namaana unapotoa sadaka
hutakiwi kutangaza huku wakiwa wamesahau
kuwa mimi ni msanii na msanii ni kioo cha jamii
natakiwa nifanye mambo mazuri na kuionyesha
jamii ili nawao waige yale mazuru niyafanyayo.
Hawa watoto wanaishi mbali sana nasehemu
wanayoishi hakuna huduma za muhimu zilizopo
karibu mfano Maduka,Hospital,Shule n.k hawana
usafiri kusema mtoto akiumwa usiku
wamuwahishe hospital je tusipo tangaza nani
atajua kuna watu wanahitaji msaada?
HIVYO NI BAADHI YA
VITANDA VYA WATOTO HAO

No comments:

Post a Comment