Tuesday, 21 October 2014

MBOWE  AKIJIACHI LIVE BILA YA CHENGA NA KIBURUDISHO CHAKE
MWANASAIKOLOJIA CHRIS MAUKI ANENA
Mtaalamu wa Saikolojia na Uhusiano ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Chris Mauki, alisema kuwa picha za Mbowe akimbusu mkewe hadharani zimemuongezea thamani kijamii kwa sababu watu wanawapenda wanaume wanaobeba majukumu ya kifamilia.

“Unadhani kwa nini Obama ni kiongozi mashuhuri sana duniani na anapendwa sana na watu, ni kwa sababu ya ile tabia yake ya kuwa karibu na familia yake. Kuna watu wanampenda Obama si kwa sababu ya nguvu kubwa aliyonayo kisiasa, ni kwa sababu anajipambanua kuwa baba bora wa familia.
“Jamii kubwa sasa inakosa upendo wa wazi kutoka kwa akina baba. Akina baba wengi wanaona kumbusu mkewe hadharani na kuwa karibu na familia siyo suala lenye maana kubwa, kwa hiyo wale ambao wanayafanya hayo waziwazi huonekana mashujaa.
“Mbowe anapongezwa kwa sababu ni shujaa kwenye jamii kwa sababu alichokifanya wengi hawakifanyi. Familia nyingi zinakosa upendo na kufanya mpaka watoto kuathirika kisaokolojia, watoto wanaharibika,” alisema Dk. Mauki na kuendelea:
“Viongozi wa kisiasa wanapokuwa wanajali familia zao, inatia hamasa kubwa. Hata kama nyumbani hawajibiki vizuri kifamilia lakini kwenye jamii anapokuwa muwajibikaji na watu wanamuona, huvutia wengi na kupendwa sana.”

No comments:

Post a Comment