Msanii wa muziki wa kizazi kipya Chid Benz amekamatwa na madawa ya
kulevya aina ya heroine na bangi akiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo.
Akizungumza Kamanda wa Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya
Tanzania, SACP, Alfred Nzowa, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kusema kuwa msanii huyo alikuwa njiani kuelekea mkoani Mbeya kwa ajili
ya shughuli zake za kimuziki.
Kamanda Nzowa amesema kuwa Chid amekutwa
na madawa hayo baada ya upekuzi wa kawaida uliokuwa ukiendelea uwanjani
hapo, ambapo jeshi la polisi linamshikilia kwa mahojiano na uchunguzi
zaidi.
Mara baada ya kupata taarifa hizo Globalpublishers iliwasiliana na Kamanda Nzoa ambaye alifunguka kama ifuatavyo:
“Ni kweli tumemkamanda Rashid Makwiro maarufu kwa jina la Chid Benz
akiwa na kete kumi na nne za madawa ya kulevya aina ya heroine pamoja na
misokoto miwili ya bangi.
“Msanii huyo alikuwa njiani kuelekea mkoani Mbeya kwa ajili ya shughuli
zake za kimuziki, na sasa amewekwa katika sehemu maalum ambayo hatuwezi
kusema ni wapi, kwa sababu za kiusalama, uchunguzi wa tukio unaendelea.”
Taarifa zilizokuwepo awali zilisema kuwa Chid alikuwa njiani kwenda
Mbeya kwa ajili ya kushiriki kwenye shoo ya Instagram Party ambayo
inatarajiwa kufanyika Jumamosi hii.
Chid ni kiongozi wa kundi la muziki la la Famila lenye makao makuu Ilala jijini Dar es salaam
No comments:
Post a Comment